- 72,309 viewsDuration: 2:16Kwa miezi kadhaa, majasusi wa Marekani walikuwa wakifuatilia kila hatua na nyendo za Rais wa Venezuela Nicolas Maduro. Kilikuwa ni kikundi kidogo cha majasusi, kilichofanya kazi pamoja na chanzo kimoja cha ndani ya serikali ya Venezuela. Walimfuatilia Maduro mwenye miaka 63 kwa kila hatua, walijua wapi analala, anakula nini, anavaa nguo gani na kwamujibu maafisa wa juu wa jeshi, waliwajua hadi "wanyama wake pendwa aliowafuga" nyumbani. Sasa baada ya kukusanya taarifa zote hizo za kijasusi, kilichofuata kikawa ni kukamilisha mpango wa kumkamata. Hilo lilitekelezwa mwanzoni mwa mwezi Disemba 2025, operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la “Absolute Resolve” ilisukwa kwa umakini mkubwa. @boshanyanje na taarifa zaidi: - - #bbcswahili #foryou #maduro #marekani #venezuela #trump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw