- 2,109 viewsDuration: 1:27Kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amewarai wapiga kura wa eneo la Nyanza kukumbuka namna alivyomuunga mkono hayati Raila Odinga katika chaguzi tatu zilizopita, akisema kuwa ndiye atakayefanikisha maono ya Raila Odinga. Akizungumza katika ziara yake kaunti ya Homa Bay, Kalonzo pia amekashifu kushambuliwa kwa msafara wake mjini Migori siku ya Alhamisi, akidai kuwa waliohusika katika uvamizi huo ni wahuni waliolipwa na viongozi wa serikali. Viongozi wa upinzani pia wamekashifu vikali maafa yanayosababishwa na ukatili wa polisi.