Skip to main content
Skip to main content

Kenya yaichapa Uganda 36-12 katika mashindano ya gofu ya Migingo Skirmishes

  • | Citizen TV
    887 views
    Duration: 57s
    Kenya imeanza kwa kishindo katika msimu wa pili wa mashindano ya gofu ya I&M Bank Katogo, Migingo Skirmishes, baada ya kuilaza Uganda kwa alama 36 kwa 12 katika uwanja wa Limuru Country Club. Migingo Skirmishes ni mashindano ya gofu ya timu yanayowakutanisha wachezaji kutoka Kenya na Uganda, huku pia yakishirikisha viongozi wa makampuni, wafanyabiashara na wapendaji wa mchezo wa gofu. Awamu ya kwanza ilifanyika katika uwanja wa Entebbe Golf Club nchini Uganda, ambapo wenyeji walitawala na kutwaa ushindi. Hata hivyo, Kenya ilirejesha makali yake ilipolipiza kisasi katika uwanja wa nyumbani jana, na hivyo kujinyakulia ushindi.