- 9,098 viewsDuration: 1:51Wanaume nchini Tanzania wanatarajia kukutana kwenye kikao rasmi cha wanaume ambacho kitafanyika Jijini Dar es salaam tarehe 2/04/2026 ambapo wanaume zaidi ya 3000 wanatarajia kukutana na kujadilia maswala mbalimbali yanayohusu ustawi wa mwanaume ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa maadili na mbinu za kujikwamua kiuchumi. Waandaji wa Kikao hiki wanasema mwanaume ameachwa licha ya mzigo mkubwa alionao wa majukumu kwenye jamii jambo linalo wasababishia msongo mkubwa wa mawazo, kikao hiki kinatarajiwa kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa kisiasa wafanyabiashara wakubwa na watu mashuhuri mbalimbali. Jukwaa hili litawaleta pia wanaume toka mataifa ya jirani ya Kenya, Uganda, Zambia na DRC ambao tayari baadhi yao wamewasili nchini Tanzania tayari kwa kikao hicho. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw