- 200 viewsKwa zaidi ya miaka hamsini, walitunga nyimbo na kupamba sherehe za kitaifa. Kina mama la Kewamoi Dancers kutoka Baringo ambao sasa wamekuwa wakongwe bado wanaendelea kutunga simulizi za uzalendo na kutumbuiza umati katika sherehe mbalimbali, kwa matumaini ya kuvutia sikio la kiongozi wa taifa. Hata hivyo, kina mama hao wanataabika kutokana na changamoto za ukongwe huku wakiitaka serikali kuimarisha hadhi ya maisha yao. Laura otieno anaangazia kundi hilo lililoshikilia utando wa uzalendo kwa miongo mitano.