- 2,384 viewsDuration: 3:06Naibu Rais Kithure Kindiki ameitetea serikali kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini akisema kuwa serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha bei hiyo inapungua. Kauli hiyo imeungwa mkono na baadhi ya viongozi wanaounga mkono serikali waliokuwa ziarani Kaunti ya Kilifi, wakisema kuwa mgogoro kati ya Marekani na Iran ndio chanzo kikuu cha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa. Mivutano ya kimataifa imechangia ongezeko la bei ya mafuta katika masoko mbalimbali duniani.