- 2,157 viewsDuration: 1:37Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani nchini (KNEC), Dkt. David Njegere, sasa anasema baraza hilo linaendelea na uchunguzi wake kufuatia kisa ambapo wanafunzi waliwavamia maafisa wa KNEC na polisi ndani ya shule hiyo. Njegere, ambaye pia alizuru shule hiyo Alhamisi wakati wa tukio hilo, amesema baraza linatarajia kutoa taarifa kamili siku ya Jumatatu. Hayo yakijiri, muungano wa walimu wa KUPPET tawi la Kisii umeibua maswali kadhaa kuhusu jinsi maafisa 15 wa KNEC walivyofika shuleni humo, ukisema kuwa walimu wakuu kadhaa katika eneo la Gusii wameripoti kuhangaishwa na maafisa wa KNEC kutoka Nairobi. Wanafunzi wawili walikimbizwa katika hospitali ya Ogembo kupokea matibabu kufuatia tukio hilo.