- 390 viewsDuration: 1:46Chama cha Kutetea maslahi ya walimu wa shule za msingi KNUT kimetoa onyo kwa Uongozi mpya wa tume ya kuuwajiri walimu nchini TSC kukoma kuwatumia wanasiasa kwenye mchakato wa kuwaajiri walimu wapya kupitia mikutano ya kisiasa. Chama hicho kupitia kwa Naibu Mwenyekiti wake wa Kitaifa Malel Lang’at kinasema hatua ya wanasiasa kutumiwa kuwaajiri walimu imesabisha walimu wengi ambao walimaliza vyuo vikuu miaka mingi iliyopita kusalia bila kazi akisisitiza haja ya taratibu za uajiri kupitia tume ya TSC kuzingatiwa wakati wa kuwaajiri walimu