Skip to main content
Skip to main content

Kuwait yakiri kudungua ndege za Marekani

  • | BBC Swahili
    22,387 views
    Duration: 12s
    Jeshi la ulinzi wa anga la Kuwait linasema kwa bahati mbaya lilidungua ndege tatu za kivita za Marekani aina ya F-15 zilizokuwa zikiruka katika operesheni zinazohusiana na Iran, kwa mujibu wa jeshi la Marekani. Wanajeshi wote sita waliokuwa ndani ya ndege hizo waliweza kujirusha nje kwa kutumia parachuti, wameokolewa salama, na hali zao zinaelezwa kuwa nzuri na thabiti. Awali, jeshi la Kuwait lilisema kuwa ndege kadhaa za kivita za Marekani zilikuwa zimeanguka nchini humo, na kwamba mazingira ya tukio hilo yalikuwa bado yanachunguzwa. Sasa, Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (US Central Command) imethibitisha kuwa ndege zake tatu za F-15, zilizokuwa zikishiriki katika Operesheni Epic Fury — operesheni ya Marekani dhidi ya Iran — zilianguka nchini Kuwait kufuatia tukio linaloaminika kuwa la kushambuliwa kimakosa na upande wao wenyewe (friendly fire). Jeshi hilo limesema wanajeshi wote sita waliokuwa ndani ya ndege hizo walijirusha nje salama na wameokolewa. Video iliyothibitishwa na BBC mapema inaonesha kile kinachoaminika kuwa ni tukio la ndege ya kivita ikidunguliwa karibu na mji wa Kuwait City. - - #bbcswahilii #iran #kuwait #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw