- 5,297 viewsDuration: 3:43Mtazamaji, msukosuko wa bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa pamoja na ongezeko la shinikizo la utumizi wa kawi safi ili kukabiliana na ongezeko la joto ulimwenguni limesukuma baadhi ya mataifa kuhimiza utumizi wa magari ya umme. Japo utumizi wa magari hayo ndio umeanza kupata kasi humu nchini, nchini China, magari ya umeme yana umaarufu mkubwa. China imejenga mtandao mkubwa zaidi duniani wa vituo vya kuchaji magari hayo yanayotumiwa na takriban wakazi milioni ishirini. Na kama anavyoarifu Boniface Barasa, uagizaji wa magari ya umeme umeongezeka barani africa kutokana na bei ghali ya mafuta na nia ya kupunguza utegemezi wa nishati zinazochafua mazingira.