Skip to main content
Skip to main content

Mahakama yaagiza ATPU, NIS na jeshi kueleza kutoweka kwa Abshir Abdi

  • | Citizen TV
    1,937 views
    Duration: 1:06
    Mahakama ya Makadara imewaagiza maafisa kutoka kitengo cha kupambana na ugaidi cha ATPU, idara ya ujasusi na jeshi kufika mahakamani Ijumaa hii kufuatia kutoweka kwa wakili Abshir Ahmedsadak Abdi. Agizo hili limetolewa kufuatia kesi inayolenga kufichua ukweli kuhusu madai ya kutekwa nyara kwa wakili huyo na aliko kwa sasa. Mahakama inawataka maafisa hao kueleza mazingira ya kutoweka kwake, huku maswali yakiendelea kuibuka kuhusu madai ya kuhusika kwa maafisa wa usalama katika tukio hilo. Wakili Abshir alitoweka Novemba mosi mwaka huu katika hali ya kutatanisha.