Skip to main content
Skip to main content

Mahakama yaamuru polisi inspekta azuiliwe siku 14 kwa uchunguzi wa mauaji

  • | Citizen TV
    2,860 views
    Duration: 57s
    Mahakama ya Milimani imewapa wapelelezi wa DCI siku 14 kumzuilia inspekta wa polisi Kenneth Kipkemboi Sang kuhusiana na mauaji ya Dkt Victoria Mutiso na wakili Kyalo Mbobu. Sang alikamatwa Eldoret baada ya kudaiwa kujificha wakati uchunguzi wa mauaji hayo ukiendelea. DCI inataka kumhoji, kufanya misako na kukusanya ushahidi zaidi. Wapelelezi pia wanamshuku Sang kwa kusaidia kupanga shambulio dhidi ya Dkt Mutiso katika barabara ya Ngong mnamo Julai 7 mwaka huu. Aidha, wanachunguza nafasi yake katika mauaji ya wakili Mbobu yaliyotokea Septemba mwaka jana. Sang anatarajiwa kufanyiwa tathmini ya afya ya akili kabla ya kusomewa mashtaka.