Mahakama Kuu imesimamisha kwa muda shughuli ya kuteua wanachama wa Bodi ya Wahandisi nchini, baada ya mlalamishi Francis Awino kupinga uhalali wa mchakato huo ulioanzishwa na Taasisi ya Wahandisi Kenya, IEK. Jaji Gregory Mutai ametoa amri zinazozuia IEK kuendelea na mchakato huo ulioanzishwa kupitia tangazo lililotolewa Agosti 25, 2026. IEK imezuiwa kuchuja, kuchagua, kuteua au kuwasilisha majina kwa Waziri wa Barabara na Uchukuzi, huku Waziri naye akizuiwa kuidhinisha, kuteua au kutangaza majina yatakayopatikana kupitia mchakato huo