- 14,457 viewsDuration: 2:27Jioni ya leo tunaanza taarifa zetu nchi jirani ya Tanzania ambako Makamu wa Rais wa taifa hilo Emmanuel Nchimbi, amejiuzulu. Nchimbi akitangaza hatua hiyo pia ametangaza kustaafu siasa. Kwenye barua yake, Nchimbi anasema alimuahidi Rais Samia Suluhu kuwa watashirikiana hadi atakapotaka kumteua makamu mwingine. Na kama Ben Kirui anavyotuarifu, kujiuzulu kwa makamu huyu wa rais chini ya mwaka moja tangu kuapishwa kunaibua maswali ya uhusiano wake na Rais Suluhu haswa wakati ambapo amekuwa akizungumzia hadharani kuhusu mageuzi ya katiba.