- 4,162 viewsDuration: 1:56Mali ya mamilioni ya pesa imeteketea baada ya moto kuchoma nyumba 5 za wageni huko Diani kaunti ya Kwale. Inadaiwa kuwa moto huo ulizuka katika eneo moja la uuzaji pombe ya mnazi maarufu mangwe na kusambaa kwa kasi kutokana na upepo uliokua ukivuma. Walioathirika na mkasa huo wanasema ni pigo kubwa kwa sekta ya utalii wakati huu msimu wa mwisho wa mwaka unakaribia.