Uvamizi wa mara kwa mara na mashambulizi ya majangili katika bonde la Kerio haukumzuia Mathew Letua kufanikisha ndoto yake ya elimu.
Letua anasema karibu alipigwa risasi miaka ya nyuma, lakini changamoto hizo hazikumzuia kuendelea na masomo hadi kufikia elimu ya juu, akihitimu kutoka mojawapo ya vyuo vikuu maarufu nchini Marekani.
Katika simulizi lake, Boniface Barasa anaripoti kuwa Letua amepokelewa kwa shangwe na wanakijiji waliovutiwa na bidii yake ya kupambana na changamoto za usalama na bado kufaulu kielimu.