- 339 viewsDuration: 2:34Waziri wa Hazina ya Kitaifa John Mbadi amewakashifu viongozi wa upinzani kwa kupinga uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za Safaricom kwa kampuni ya Vodacom, akisema zaidi ya shilingi bilioni 200 zitakazopatikana kupitia mpango huo zitasaidia kufadhili miradi ya maendeleo nchini. Akizungumza Kisumu, Mbadi pia aliwataka Wakenya kupuuza viongozi hao, akidai wanaingiza siasa katika mpango huo wa serikali.