- 376 viewsDuration: 1:20Makala ya nne ya mbio za nyika za Chepsaita yamezinduliwa katika kijiji cha Chepsaita, eneo bunge la Turbo kaunti ya UasinGishu. maandalizi kabambe yameanza kabla ya mbio hizo kufanyika tarehe tano Desemba. Muasisi wa Mbio hizo ambaye pia ni msaidizi wa rais Farouk Kibet, amewataadharisha wanariadha dhidi ya utumizi wa dawa za kusisimua misuli,akisema hulka hiyo itazima ndoto zao.Lengo kuu la mbio hizo ni kufadhili elimu ya wanafunzi kutoka familia za mapato ya chini.