- 13,017 viewsDuration: 2:41Mwakilishi wadi wa Kemeloi-Maraba katika Kaunti ya Nandi amejipata matatani kufuatia vitisho alivyotoa dhidi ya wanaopinga azma ya Rais William Ruto kuchaguliwa kwa muhula wa pili. Mwakilishi wadi wa Kemeloi-Maraba, Truphosa Kuto, alinukuliwa akiwaonya wakazi kuwa watakaomuunga mkono mgombea mwingine wa urais wataondoka kaunti hiyo. Haya yanajiri huku Mbunge wa zamani Rueben Ndolo akijiwasilisha mbele ya Tume ya Uwiano (NCIC) kwa madai ya kuwakusanya wahuni kuvuruga mkutano uliofanyika huko Siaya. Ben Kirui na kina cha taarifa hiyo.