Skip to main content
Skip to main content

Mechi za ligi zavuruga maandalizi ya Emerging Stars kukabiliana na Ivory Coast

  • | Citizen TV
    1,486 views
    Duration: 29s
    Msongamano wa mechi za ligi, uliosababishwa na kuchelewa kuanza kwa msimu, umeathiri maandalizi ya timu ya taifa ya chipukizi, Emerging Stars, kabla ya mechi muhimu dhidi ya Ivory Coast wiki ijayo. Timu hiyo iliripoti kambini siku tatu zilizopita, lakini mazoezi yake yatavurugwa na wachezaji kurejea katika vilabu vyao kwa mechi za ligi wikendi hii. Kocha Anthony Kimani anasema mpangilio wa sasa hauipendelei timu hiyo, kwani hakuna viwanja vya mechi jijini Nairobi. Wachezaji hao watalazimika kusafiri nje ya mji, kucheza dakika 90 kwa timu zao na kurejea Nairobi kambini Jumatatu jioni. Hali hii haitawapa muda wa kutosha wa kupumzika, huku mechi dhidi ya Ivory Coast ikitarajiwa kufanyika Jumatano. Wachezaji wengi walioitwa kutoka vilabu vya Uropa pia hawatapatikana hadi baada ya mechi zao za wikendi. Licha ya changamoto hizo, Kimani ana matumaini ya kuona timu yake ikifanya vyema dhidi ya Ivory Coast baada ya kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Tanzania, ambapo walipoteza mabao 3-1 jijini Dar es Salaam.