- 389 viewsDuration: 1:52Katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini Seth Panyako amedokeza kuwa bado hakujakuwa na muelekeo wa kusitisha mgomo wa wauguzi katika hspitali za kitaifa na za kaunti. PAanyako amesema wauguzi bado wanalilia mkataba wa CBA ambo serikali nyingi za kaunti zimedinda kuidhinisha. Malalamishi hayo yanajiri siku moja baada ya kamati ya afya katika baraza la magavana kukutana jana na naibu rais Prof. Kithure Kindiki na kudai kuwa matakwa ya wauguzi hayawezi kuafikiwa kikamilifu kwa sasa.