- 12,898 viewsDuration: 1:29Kizaazaa kimetokea Manyatta, Kaunti ya Embu, baada ya mjane na watoto wake kufika kwenye mazishi ya mumewe na kupata tayari amezikwa. Patashika hiyo imeshuhudiwa baada ya familia ya Simon Ndwiga kufanikisha mazishi yake kabla ya saa tatu asubuhi ya leo. Mkewe Mercy Wanja aliwasili katika boma la mumewe na kupata kaburi lake tayari limefunikwa. Haya yanajiri baada ya familia ya marehemu kupata idhini ya mahakama ya kumzika, licha ya kesi iliyowasilishwa na Wanja ya kuzuia mazishi hayo, miezi miwili tangu mumewe afariki.