- 1,004 viewsDuration: 1:23Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 27 amefikishwa katika mahakama ya Garissa kwa tuhuma za ulanguzi wa binadamu kaunti hiyo. Mohammed Abdikarim ambaye ni mhudumu wa tuk tuk mjini Garissa, anakabiliwa na kosa la kujaribu kuwatafutia Zakaria Badel Kahir na Abdirizak Hirsi Farah namna ya kufika jijini Nairobi kunyume cha sheria wote wakiwa kutoka kambi ya wakimbizi la Hagadera. Mshukiwa alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu mkazi Shadrack Otuke akisema alichukulia wawili hao kama wateja wa kawaida. Hakimu alikubali ombi la upande wa mashtaka na kuamuru mshukiwa kusalia rumande kwenye gereza la Garissa hadi jumatatu tarehe 15 mwezi huu wakati kesi itakaposikizwa tena.