Skip to main content
Skip to main content

Mwanafunzi Nakuru asalia nyumbani kutokana na ugonjwa wa muda mrefu

  • | Citizen TV
    3,601 views
    Duration: 3:00
    Mwanafunzi wa Gredi ya Kumi kutoka kaunti ya Nakuru amelazimika kusalia nyumbani kutokana na ugonjwa usio wa kawaida unaosababisha mguu wake wa kulia kuvimba kila anapotembea. Kwa zaidi ya miezi sita, Debra Njiiri, mwanafunzi wa Moi Forces Academy, hajafika shuleni huku wenzake wakiendelea na masomo. Familia yake inasema imehangaika kutafuta matibabu kwa zaidi ya miaka kumi bila mafanikio, hali ambayo imeendelea kumzuia kuishi maisha ya kawaida ya masomo na maendeleo ya elimu. Maryanne Nyambura anaripoti zaidi.