Skip to main content
Skip to main content

Mwanaharakati awasilisha ilani ya maandamano ya Saba Saba

  • | Citizen TV
    5,195 views
    Duration: 1:12
    Mwanaharakati mmoja amewasilisha ilani ya kufanya maandamano ya Saba Saba siku ya Jumanne, ambapo zaidi ya watu elfu tatu wanatarajiwa kushiriki jijini Nairobi. Ilani hiyo iliyowasilishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi imeorodhesha masuala watakayozingatia, ikiwemo ongezeko la visa vya utekaji nyara, uchunguzi wa madai ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na uzingatiaji wa sheria kwa jumla. Wakati uo huo, Mbunge wa Makadara George Aladwa alisema kuwa chama cha ODM hakitashiriki maandamano hayo na kuzitaka asasi za usalama kuwajibika Jumanne.