- 763 viewsDuration: 4:12Katika makala yetu ya Mwanamke Bomba leo, tunamuangazia Veronica Mwende, aliyebobea katika kazi ya kuchomelea magari na bidhaa za chuma. Veronica, anayefanya kazi katika karakana mbili tofauti katika mtaa wa Njiru, viungani mwa jiji la Nairobi, ni mama wa watoto wawili. Anasema aliamua kujifunza kazi hiyo ili kukidhi mahitaji yake na ya wanawe baada ya maisha kuwa magumu kufuatia janga la corona.