- 2,714 viewsDuration: 1:23Kinara wa Chama cha People's Party na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ameukosoa mfumo unaopendekezwa na kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, wa kumteua atakayepeperusha bendera ya upinzani, akionya kuwa misimamo yake migumu inaweza kumpa Rais William Ruto muhula wa pili. Nyoro, ambaye amemtaka Gachagua kupanua mawazo na kutoangazia ushawishi wa vinara binafsi katika azma hiyo, hata hivyo, amemuunga mkono katika wito wa kuungana na kutafuta uungwaji mkono mpana ili kumwondoa Rais Ruto mamlakani. Alikuwa akizungumza katika vikao na wakazi wa maeneo bunge ya Kangema na Mathioya.