Gavana wa Kajiado, Joseph Ole Lenku, amezindua rasmi chama cha Forum for Economic Development Agenda (FEDA), katika uzinduzi uliofanyika kwa wakati mmoja katika kaunti za Kajiado, Narok na Marsabit.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Kajiado Kusini, Samuel Sakimba, alitetea haki ya Gavana Lenku ya kuunda chama hicho, akipuuza wakosoaji wa kisiasa.
Ole Lenku alisisitiza kuwa FEDA itawahudumia Wakenya wote, akitangaza kuwa maeneo yaliyotengwa hayatatumika tena kama vyombo vya biashara ya kisiasa.