Skip to main content
Skip to main content

Polisi wachunguza kifo baada ya vurugu Kisii

  • | Citizen TV
    4,663 views
    Duration: 3:18
    Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanaume mmoja amefariki baada ya kundi la wahuni kuvamia msafara wa mrengo wa Linda Mwananchi katika eneo la Keumbu, Kaunti ya Kisii. Kijana huyo wa miaka 36, Vincent Osiemo, alianguka kutoka kwenye gari moja la mwanasiasa alimokuwa ndani baada ya kushambuliwa kwa mawe. Aidha, Idara ya Upelelezi imemtaka Mbunge wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, kuandikisha taarifa huku watu wanane wakizuiliwa kufikia sasa. Chrispine Otieno anaarifu kutoka Kisii.