Skip to main content
Skip to main content

Polisi wachunguza kifo tata cha nyanya mwenye miaka 86 Loresho

  • | Citizen TV
    6,653 views
    Duration: 1:10
    Polisi katika kituo cha Gigiri wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo tata cha mwanamke wa miaka 86 nyumbani kwake mtaani Loresho siku ya Ijumaa. Kwa mujibu wa wakili wa marehemu, nyanya huyo anadaiwa kushambuliwa ndani ya nyumba yake, na kufariki muda mfupi baadaye. Watu sita wanaohusishwa na kisa hicho wamekamatwa na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri. Miongoni mwao ni jamaa wawili wa familia ya marehemu ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho.