- 5,669 viewsDuration: 3:04Polisi katika eneo la Mathare 3C jijini Nairobi wamelazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya kundi la wakazi ambao kwa siku ya pili mfululizo wameandamana wakitaka kuachiliwa kwa mwanasiasa na mfanyabiashara Joel Kariuki, anayeaminika kutekwa nyara. Inasemekana kuwa tangu Alhamisi Kariuki hajulikani aliko, baada ya kubebwa na watu ambao wakazi wanadai walijitambulisha kama maafisa wa polisi. Familia ya mfanyabiashara huyo imetaka aachiliwe mara moja au afikishwe mahakamani iwapo ana tuhuma zozote za kujibu. Kamau Mwangi anaripoti zaidi.