- 14,582 viewsDuration: 3:03Mwigizaji maarufu Regina Wangui Macharia, maarufu Regina Re, pamoja na kakake na bintiye ni miongoni mwa watu wanne wanaozuiliwa kuhusiana na mauaji ya mama yao. Mahakama ya Kibra imekubali ombi la maafisa wa uchunguzi la kuwazuilia washukiwa hao kwa siku zaidi ili kukamilisha uchunguzi. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 86 aliuawa nyumbani kwake katika mtaa wa Loresho, Nairobi. Mary Muoki anaaarifu.