- 2,384 viewsDuration: 3:04Rais William Ruto ametangaza mpango wa mageuzi katika sekta ya kahawa akisema wakulima watalipwa kwa chini ya siku tano baada ya kufikisha kahawa yao sokoni. Akizungumza kaunti ya Kirinyaga County leo, Rais Ruto pia alisema wakulima watalipwa deni la shilingi bilioni 2 katika bajeti ya mwaka ujao wa kifedha. Na kama anavyoarifu Emmanuel Too, Rais Ruto pia aliwakashifu wabunge walioipinga mswada wa fedha wa mwaka 2026, akisema walipotoshwa na viongozi wao wa kisiasa.