- 3,963 viewsDuration: 3:08Tanzia na majonzi ziligubika Familia za watu saba waliofariki kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Nyanja kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret, zilikumbwa na majonzi makubwa zilipofika katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Londiani kutambua miili ya wapendwa wao. Miongoni mwa waliofariki ni mfanyakazi wa IEBC na mwalimu waliokuwa wakisafiri kutoka Nakuru kuelekea Eldoret wakati gari lao lilipogongana na trela.