Waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi amesisitiza kwamba pendekezo la uuzaji wa hisa asilimia 15 za serikali kutoka kampuni ya Safaricom lilifanywa kulingana na sheria. Akihutubia wanahabari mjini Kisumu mapema leo, Mbadi alisema kwamba serikali itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu uliositisha uuzaji wa hisa hizo za serikali kwa kampuni ya Vodacom, huku akisisitiza kwamba taifa lina haki la kujiendeleza kupitia miradi ya maendeleo kupitia uwekezaji mwafaka unaotokana na uuzaji halisi wa rasilmali za serikali.