Serikali inaanzisha mpango wa mafunzo ya bure ya kidijitali unaolenga kuwafikia zaidi ya vijana laki sita, wakiwemo wanawake na watu wenye ulemavu, ili kuwawezesha kupata kandarasi za serikali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo hapa Nairobi, Katibu katika Idara ya Biashara Ndogo, Susan Mang’eni, amesema watakaokamilisha mafunzo hayo watapewa vyeti.
Aidha, wale ambao hawajasajili biashara zao wataunganishwa na huduma za usajili wa biashara, huku serikali ikiandaa mfumo utakaowawezesha wafanyabiashara kulipwa ndani ya siku 60 baada ya kusambaza bidhaa au kutoa huduma.