- 465 viewsDuration: 1:30Serikali kupitia wizara ya kilimo na mifugo imeanza hatua za kujenga upya mabwawa ya kikoloni humu nchini kwa lengo la kuwasadia wakulima Katika unyunyizaji wa mashamba yao hatua ambayo itaboresha uzalisha wa vyakula . Akizungumza katika uzinduzi wa ukarabati wa mradi wa bwawa la kivuno Kipkelion Mashariki Katibu Katika wizara hiyo Dr. Paul Ronoh amesema ujenzi wa mabwawa matano ya kikoloni tayari umeratibwa kuanza hivi karibuni ili kuwahakikishia wakazi wa Kaunti hiyo maji ya kutosha.