Serikali imetakiwa kutoa muongozo wa kitaaluma kwa watahiniwa wa kidato cha nne ili kuwasaidia kuchagua taaluma zinazofaa na kuendana na mahitaji ya soko la kazi la kisasa.
Wito huo umetolewa na wazazi na wadau wa elimu wakati wa hafla ya kukamilika kwa mafunzo ya miezi mitatu yaliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa masuala ya afya KEMRI kwa wanafunzi wanagenzi, lengo likiwa ni kuwapa mwongozo wa kuchagua masomo ya sayansi na taaluma mbalimbali.
Wazazi wameshauri serikali kuiga mpango huo na kuupanua ili kuwafikia wanafunzi wengi zaidi, wakieleza kuwa ni wanafunzi 12 pekee kati ya zaidi ya 1,000 walioomba walionufaika na nafasi hiyo.