- 2,392 viewsDuration: 1:23Katibu wa Michezo, Elijah Mwangi, ametetea mpango wa serikali wa kuleta timu mbili za soka za kigeni, Bayern Munich na Ajax, zitakazoshiriki mashindano ya ufunguzi wa Uwanja wa Raila Odinga Januari mwaka huu. Mwangi amesema serikali haitatumia fedha za walipa ushuru kufanikisha mpango huo, kwani imejipanga kushirikiana na kampuni binafsi na wadau wengine wa michezo kusimamia gharama ambazo wachezaji hao watatumia. Kulingana naye, kuleta timu hizo kutaimarisha utalii, kupiga jeki biashara katika jiji kuu la Nairobi na kaunti jirani, pamoja na kukuza vipaji.