- 354 viewsDuration: 2:51Shule kadhaa katika eneo la Gusii zimeanza kutumia majiko ya stima pamoja na teknolojia nyingine za kisasa ili kuboresha na kurahisisha huduma za upishi kwa mamia ya wanafunzi. Mvumbuzi kijana Hykarus Ondimu kutoka kijiji cha Nyamemiso mjini Kisii amesema anatumia vyuma na ujuzi wake katika teknolojia ya nishati ya jua kuunda majiko hayo, hatua inayochangia matumizi bora ya nishati na kupunguza gharama za upishi katika taasisi za elimu.