- 7,661 viewsDuration: 2:30Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, mmoja wa vinara wa LINDA Mwananchi, amekanusha madai ya Rais William Ruto kwamba mrengo huo unafadhiliwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Akizungumza na vijana wanaolenga kugombea viti katika uchaguzi ujao, Sifuna amemtaka Rais Ruto kutoa ushahidi wa madai hayo, huku akimshtumu kwa kuupaka tope upinzani na kusema hauna ajenda ya kuendeleza Kenya.