- 9,187 viewsDuration: 2:58Simanzi nzito na majonzi vilitanda katika uwanja wa Gilgil wakati wa ibada ya wafu ya wanafunzi 16 waliofariki kwenye mkasa wa moto wa Utumishi Girls Academy. Mamia ya waombolezaji waliungana na familia za wanafunzi hao na kueleza vifo hivyo kuwa vya kusikitisha na kuvunja moyo. Ingawa mmoja wa wanafunzi waliofariki tayari amezikwa, familia za waliosalia zilikabidhiwa miili kwa ajili ya mazishi.