Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Erastus Ethekon amesema kwamba tume hiyo itapiga marufuku wanasiasa na wawaniaji wa wadhifa mbali mbali, watakaopatikana na hatia ya kutekeleza ghasia na fujo wakati wa kampeini za uchaguzi. Akizungumza katika mkutano kuhusu maandalizi ya usalama wa uchaguzi mkuu ujao jijiji Nairobi, Ethekon atangaza kwamba ukosefu wa vitambulisho miongoni mwa Wakenya ni changamoto kuu katika usajili wa wapiga kura nchini huku akitaka swala hilo liangaziwe na idara husika za serikali. Mkutani huo pia ulihudhuriwa na waziri wa usalama Kipchumba Murkomen