Skip to main content
Skip to main content

Tundu Lissu akabiliwa na mashataka mengine. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    24,022 views
    Duration: 28:16
    Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, anakabiliwa na mashtaka mengine matatu baada ya kuhitimishwa kwa kesi ya hivi karibuni iliyomkuta na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela. Lissu anatarajiwa kufikishwa mahakamani Alhamisi wiki ijayo kujibu mashtaka matatu ya madai ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube, makosa yanayokiuka sheria ya makosa ya mtandao nchini humo. Kesi hiyo inahusiana na matamshi ambayo anadaiwa kuyachapisha kupitia YouTube Aprili 3 mwaka jana. Hati ya mashtaka inaonyesha kuwa shtaka la makosa ya mtandao liliwasilishwa Aprili 10, 2025, siku hiyo hiyo alipofunguliwa mashtaka ya uhaini na uchochezi kutokana na matamshi aliyoyatoa katika mkutano wa kisiasa. #tundulissu #tundulissumahakamani #Zelensky #putin #Trump #BBCSwahili #Tiktok Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw