Skip to main content
Skip to main content

UASU yaitaka serikali kutekeleza kikamilifu mkataba wa makubaliano wa wahadhiri wa vyuo vikuu

  • | Citizen TV
    1,393 views
    Duration: 1:52
    Muungano wa wahadhiri wa vyuo vikuu UASU unaitaka serikali kutekeleza mkataba wa makubaliano kwa ukamilifu badala ya kuendelea kuwachezea shere. Akizungumza mbele ya kamati za bunge kuhusu leba na elimu , katibu mkuu wa UASU daktari Constatine Wesonga , amesema wahadhiri walisitisha mgomo ili kupisha mazungumzo ya kutatua suala la mishahara kabisa, baada ya serikali kulipa shilingi bilioni 20 za madeni ya wafanyakazi wa vyuo vikuu.