- 4,384 viewsDuration: 2:40Kinara wa chama cha PLP ambaye pia ni wakili Martha Karua amepigwa marufuku kuingia nchini Uganda. Haya yamejiri baada ya Karua kuzuiliwa katika uwanja wa ndege wa Entebbe alipokuwa akielekea Kampala kumuona wakili mwenza wa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye. Chama cha mawakili cha Afrika Mashariki sasa kinasema kitashtaki serikali ya Uganda huku kikitafuta maelezo kuhusu sababu za kumpiga marufuku Karua.