Skip to main content
Skip to main content

Uhaba wa maziwa waripotiwa nchini

  • | Citizen TV
    2,527 views
    Duration: 3:17
    Uhaba wa maziwa umeendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku baadhi ya maduka ya rejareja jijini Nairobi na viungani mwake yakikosa bidhaa hiyo. Wafanyabiashara wanasema usambazaji wa maziwa umepungua kwa kiasi kikubwa, huku baadhi ya maduka yakiripoti ongezeko la bei la kati ya shilingi tatu na tano kwa pakiti ndogo ya maziwa. Bodi ya Maziwa nchini imesema hali hiyo ni ya muda na inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya msimu.