Skip to main content
Skip to main content

Ukame waharibu mazao Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    560 views
    Duration: 3:26
    Wakulima katika Kaunti ya Trans Nzoia wanakadiria hasara kubwa baada ya mazao yao kuharibikia shambani kutokana na ukosefu wa mvua. Kwa mujibu wa wizara ya kilimo, zaidi ya ekari 50,000 za mazao zimeharibikia shambani kaunti hiyo, hali ambayo inatilia shaka uzalishaji wa kutosha wa chakula msimu huu. Wakulima sasa wanairai serikali kupunguza zaidi bei ya pembejeo ili waweze kurejea mashambani na kukuza upya chakula.