Skip to main content
Skip to main content

Uongozi wa kanisa la ELCK wataka serikali iimarishe SHA

  • | Citizen TV
    674 views
    Duration: 1:39
    Uongozi wa kanisa la ELCK nchini wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa hilo nchini Dkt. Joseph Ochola, wameishauri serikali ya Rais William Ruto kuiangalia bima ya SHA kwa kina, wanayosema imewatatiza wananchi wengi wanaotafuta huduma hospitalini. Wakizungumza kwenye ibada ya uzinduzi wa jengo jipya katika makao makuu ya kanisa hilo kule Nyamira, viongozi hao wamemshauri Rais William Ruto kuangazia madai ya ufisadi na ufujaji wa pesa za umma kupitia bima hiyo na idara nyingine za serikali.