Skip to main content
Skip to main content

Usalama waimarishwa jijini Nairobi kabla ya kongamano la Africa Forward

  • | KBC Video
    3,631 views
    Duration: 3:19
    Huduma ya taifa ya polisi imeimarisha usalama kabla ya kongamano la siku mbili la Africa Forward la mwaka huu litakaloandaliwa Jumatatu na Jumanne wiki ijayo. Kamanda wa polisi katika eneo la kaunti ya Nairobi Issa Mohamud, aliyezungumza kwa niaba ya Inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja alisema kuwa usalama umeimarishwa huku doria zikitekelezwa kwa saa 24 kwa siku na maafisa wa polisi wakilinda usalama katika maeneo yote ya umma kote nchini. Huduma hiyo pia ilitangaza kuvurugwa kwa shughuli za uchukuzi kwa muda kwenye barabara kuu wakati wa kongamano hilo la siku mbili litakaloandaliwa kwa pamoja na rais William Ruto wa Kenya na mwenzake wa ufaransa Emmanuel Macron. Barabara zitakazoathirika ni pamoja na ile ya Mombasa road, Thika superhighway na ile ya Kiambu miongoni mwa nyingine. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive